


Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars,Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka beki wa timu ya Rwanda, Nzeyimana Hussein katika mchezo uliopigwa jana ndani ya dimba la Taifa. Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kuikandamiza Burundi mabao 2-0.

Nurdin Bakari (mfungaji wa magoli mawili ya kili stars) akijiandaa kuachia shuti kali ambalo ilikuwa almanusra kupachika bao la tatu.

Mshike mshike katika lango la timu ya Burundi ambapo golikipa wake,Niyonkuru Vladimir aliweza kuizuia hatari hiyo.

Salum Machaku wa Kilimanjaro Stas, akiwa yeye na kipa wa Burundi, lakini kwa mshngao wa wengi, alijikuta akipiga bonge la shuti ambalo lilikwenda nje, huku golikipa wa Burundi akilisindikiza kwa macho.


Mashabiki wakishangilia bao la pili la Kilimanjaro Stars dhidi ya Burundi katika Uwanja wa Taifa Jana.
No comments:
Post a Comment