Monday, November 16, 2009

MAMA SALMA KIKWETE

Imekuwa kawaida kwa Mama Salma Kikwete kupenda kuzungumza na Watoto wa Shule kila mahala awakutapo, na mara nyingi amekuwa mama wa mfano katika kuwaasa wanafunzi hao hususan wale wa kike, kuachana na masuala ya anasa katika umri wao na badala yake wazingatie masomo zaidi!
hapa Mama huyu ambaye ni mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anazungumza na Mwanafunzi huyu ambaye alimkuta mkoani Lindi akiwa ametinda nyusi zake na kumwambia kuwa achane na mambo hayo na badala yake azingatie masomo zaidi!!!, si unajua tena vishawishi ni vingi ambavyo vinaweza kumvuta mwanamme akajikuta akirusha kete kwa binti huyu, lakini Mama amelistukia hilo

No comments: