Sunday, December 5, 2010

Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Towero cha Manispaa ya Morogoro , Rajab Athuman ‘ Roja’ akionyesha umahiri wa kucheza na nyoka aina ya chatu , wakati wa onyesho la wasanii wa Kikundi hicho , siku ya Mahafali ya 17 ya wahitimu wa Ualimu wa Ufundi Stadi , ngazi ya Stashahada na Cheti katika Chuo cha Mafunzo ya Ualimu VETA Morogoro, iliyohudhuriwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulungo, mjini Morogoro.
Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Towero cha Manispaa ya Morogoro , Rajab Athuman ‘ Roja’ ambaye ni bingwa wakucheza na nyoka aina ya chatu , akiwaonesha baadhi ya wananchi sehemu aliyoumwa na Chatu, baada ya kumaliza onyesho lao. Bahati nzuri chatu huyo hana sumu kali, hivyo alinusurika. Na hii alisema si mara ya kwanza kung'atwa. Picha na mdau John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro.


No comments: