Thursday, November 13, 2008

DAY 4.

RAFIKI SI LAZIMA AWE MWAFRIKA TU!!!, LILIAN HAPA ANAONEKANA AKIWA AMEPOZI NA MKE WA BALOZI WA FINLAND SIKU ALIPOWAANDALIA PART WASHIRIKI WA WORKSHOP YA INTERNET TRAINERS, NOVEMBER 11,2008.














DAY 3.- JOURNALISTIC RESARCH ASSIGNMENTS THROUGH THE INTERNET
Katika somo la jana, tuliweza kujifunza namna ya kuweza kutafuta habari mbalimbali kwa kupitia katika mitandao mbalimbali ambayo inapatikana katika website ya Google.
Mwalimu alielekeza kuwa katika website hiyo, unaweza kucheza nayo na ukaweza kujipatia vitu vingi ambavyo binafsi hukutarajia kuvipata.
Kwa mfano, tuliweza kupata majina ya marais wa nchi mbalimbali, sanjari na wasifu wao, pia tuliweza kuona namna tunavyoweza kupata takwimu kwa mfano za maradhi kama malaria, ambapo hapa tuliiangalia wilaya ya Karagwe iliyoko mkoani kagera.
Hata hivyo Mwalimu alitoa angalisho kuwa, si vyema kuziamini moja kwa moja takwimu ambazo zimo katika mtandao kama waandishi wa habari.
Bali alielekeza pia kwa kupitia website ya google, waweza kuingia katika mtandao wa Wiki pedia na hapo waweza kupata pia njia za mawasiliano mengine kama namba za simu za wahusika ambao unaweza kuwasiliana nao na ukaweza kuoanisha habari ya takwimu zako ulizozipata katika mtandao na zile ambazo utaelezwa na muhusika moja kwa moja.
Hata hivyo tuliona pia kuwa Internet ni moja ya nyenzo muhimu katika uandishi wa habari hasa katika nyakati hizi tulizonazo sasa, kwa kuwa inakuwezesha na kukurahisishia kazi ya uandishi hasa kama utakuwa ukitazama zaidi mitandao ya mashirika ya habari ya nje ambapo utaweza kujipatia habari mbalimbali toka ulimwenguni kote kwa lugha mbalimbali Kiswahili kikiwemo, hususani katika website ya BBC, Inter Press Service (IPS), aljazeeral, CNN Reuters, All Afica.com African Jounal on ward (AJOL). Misa workshop.
Pia tuliweza kujifunza namna ya kutengeneza na kuzipanga habari katika blog zetu kwa kuona mifano ya w engine ambao tayari blog zao zinasomwa na watu wengi kwa sasa.
Kwa mfano Tanzania hivi sasa blog ya mwandishi Muhidin Issa Michuzi imeonekana kutembelewa na watu wengi.
Pia tulitazama blog ya xe.com, hello in my language, Kenya unlimited blog global voice wiki na nyingine nyingi ambazo nikiziandika zote hapa nadhani tutakesha.
So kutokana na mafundisho ya jana ambayo ilikuwa ni siku ya tatu toka kuanza kwa masomo hayo hapa Tanzania Global Development Learning Centre TGDLC), ninazidi kujifunza mambo mengi ambayo nilikuwa siyafahamu hapo awali.

No comments: