Tuesday, November 16, 2010



RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA MH. MIZENGO KAYANDA PINDA, MBUNGE WA JIMBO LA KATAVI, KUWA WAZIRI MKUU, KWA MUJIBU WA TANGAZO LILILOSOMWA BUNGENI SASA HIVI NA SPIKA WA BUNGE MH. ANNE MAKINDA.
ZOEZI LINALOFUATA SASA NI WABUNGE KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUUAMBAPO MWANASHERIA MKUU MH. FREDERICK WEREMA ANATOA HOJA YA KUWAOMBA WAHESHIMIWA WABUNGE WAMTHIBITISHE AMBAPO ITAPIGWA KURA YA PAPO KWA PAPO NA BAADAYE UTAFUATIA UCHAGUZI WA NAIBU SPIKA AMBAYE ATAJULIKANA LEO PIA.
WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUAPISHWA KESHO IKULU NDOGO YA CHAMWINO, IKIWA NI HATUA YA KWANZA KABLA YA KUTANGAZWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI. HATUA HII INAKAMILIKA BAADA YA RAIS KUKAA NA KUSHAURIANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.
BARAZA HILO JIPYA LINATARAJIWA KUTANGAZWA IJUMAA
KURA ZILIZOPIGWA: 328
KURA ZA NDIO: 277 (85.4%)
KURA ZA HAPANA: 49 (14.9%)
KURA ZILIZOHARIBIKA 2 (0.2%)

No comments: