Tuesday, December 7, 2010


Mausoleum (kaburi maalumu) ambapo mwili wa aliyekuwa Rais wa Kwanza na muasisi wa Taifa la Malawi Ngwazi Dr Hastings Kamuzu Banda umehifadhiwa. Huu mwili umewekwa dawa ili usiharibike kwa muda wa miaka 99. Kamuzu alifariki mwaka 1997 tarehe 25 Novemba na baadaye mwili kuhifadhiwa kwenye hiyo mausoleum. Kufuatana na maelezo ya msimamizi wa eneo hilo, inasemekana baada ya kufariki Rais wa pili Bakili Muluzi pamoja na kuahidi kuwa angelijenga Mausoleum hiyo hakutimiza ahadi yake hiyo kwa muda wote wa miaka 10 ya uongozi wake. Rais wa tatu Ngwazi Profesa Bingu wa Mutharika ndiye aliyesimamia ujenzi wa kituo hicho kilichojengwa kwa takaribani miezi 18.
Mausoleum hiyo inatunzwa vizuri sana na mandhari yake yanavutia na pana bustani yenye miti na maua ya kupendeza. Upandapo ngazi kwa nje kuna picha kubwa ya Ngwazi. Pembeni kwa upande wa kushoto kuna majengo ya Bunge na upande wa kulia kwa sasa wanajenga kituo cha mikutano cha kimataifa na hoteli ya 5 star. Ni dhahiri eneo hilo litakuwa la kuvutia kwa kila hali. Pale ukifika msimamizi anakueleza historia ya Kamuzu. Pamoja na kuwa alionekana ni Dikteta aliyesababisha Wamalawi wengi waihame nchi bado wameamua kumpa heshima yake kama Rais wa Kwanza na muasisi wa taifa lao. Historia haiwezi kufutwa.
Mausoleum hiyo imezungukwa na nguzo nne ambazo zinakumbushia misingi mikuu minne ambayo Kamuzu alioitumia kuiongoza nchi ya Malawi. Misingi hiyo ni UNITY, LOYALTY, OBEDIENCE na DISCIPLINE.


Mheshimiwa Patrick Tsere balozi wa Tanzania nchini Malawi alipofika kupatembelea na kupewa maelezo na msimamizi wa eneo hilo, kwenye kaburi ambapo mwili umelazwa. Kwa nyuma kwenye ukuta utaona official potrait ya Kamuzu akiwa ameshika usinga ambao kwa mara ya kwanza alipewa na marehemu Jomo Kenyatta Rais wa nchi ya Kenya. Kwa mujibu wa official hostess mama Cecilia Kadzamira, Kamuzu alikuwa anazo fimbo za usinga zipatazo 19 wakati wa uhai wake. Fimbo ya usinga ni symbol of authority and power.




No comments: