Thursday, January 6, 2011


Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Cyril Chami (shoto) na naibu wake Mh. Nyalandu, akiongea kabla ya kupaa kuelekea India, Tanzania inaweka mikakati ya kupata wawekezaji katika uzalishaji wa chuma na kilimo kutoka nchini India.

Akizungumza jijini Dar es salaam juzi jioni kabla ya kusaifiri kwa ziara ya siku saba nchini India, waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami alisema kuwa safari yake na viongozi wengine nchini India itakuwa na manufaa makubwa kwa taifa.
“tunakwenda kwa mwaliko wa Chamber of Commerce ya jimbo la Marakshi kwa ajili ymaonyesho ya biashara, lakini wao ni wawekezaji wakubwa katika chuma, kwa miradi yetu kama ya Mchuchuma na Liganga tunaweza kufanikiwa”.
Dk Chami alisema mbali na uwekezaji katika uchimbaji wa chuma pia katika kilimo Tanzania imekuwa ikifanya bishara kubwa na India, lakini kwa sasa wanatazamia kupata wawekezaji wanaoweza kuboresha mazao yetu yakaongezewa thamani hapa nchini.
“India ndio wateja wakubwa wa korosho zetu lakini kwa sasa zidhani kama tuna haja ya kuwauzia zikiwa bado ghafi, ni lazima tuongeze thamani na tuuze zikiwa zimetengenezwea ili kupoata faida zaidi” alisema.
Ushirikiano wa kibiashara kati ya India na Tanzania umekuwa ukiongezeka kwa kasi na ni nchi pekee ambayo biashara baina yake na Tanzania inapanda mwaka hadi mwaka.
Dk Chami alisem akuwa sasa hivi ni wakati muafaka wa kuweza kupata wawekezaji ili kufaidi keki hiyo ambapo Afrika ikiwa na watu zaidi ya asilimia 15 lakini ni asilimia moja tu ya uwekezaji duniani huja Afrika.
Pia alifafanua kuwa katrika asilimai moja hiyo ni nchi chache zinazonufaika zaidi zikiwemo Nigeria, Misri na Afriak Kusini na iliyobaki nduio hubakia kw anchi kama za Tanzania na nyinginezo.
Alisema kikubwa kw ayeye na ujumbe wake ni kupata wawekezaji wakubwa ambao wataleta fedha nyingi na teknolojia nchini ili kuwez akukuza biashara na viwanda vya ndani.

No comments: