Tuesday, December 7, 2010



Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Bw. David Mgwassa (katikati) akihutubia wakati wa hafla ya wafanyakazi kusherehekea uzalishaji na kuvuka malengo ya mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kiwanda hicho, Dar es Salaam wikiendi ilopita. Kushoto ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa TDL, Joseph Chibehe na kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Ufundi, Aranyael Ayo pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala, Mustafa Nassoro.



Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mustafa Nassoro, akielezea siri ya mafanikio ya kiwanda hicho,wakati wa hafla ya wafanyakazi kusherehekea uzalishaji na kuvuka malengo ya mauzo ya vinywaji vinavyozalishwa na kiwanda hicho. Kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa TDL, David Mgwassa na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kiwanda hicho, Joseph Chibehe.



Wafanyakazi wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limite (TDL), wakifungua kinywaji aina ya Chamdol ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kuvuka lengo la mauzo ya bidhaa za kiwanda hicho. Kutoka kushoto ni Halima Nassor, Majid Shomari na Elizabeth Mhamiji.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), wakigongeana chupa na glasi zenye vinywaji na viongozi wa kiwanda hicho kufurahia mafanikio ya kuvuka lengo la mauzo ya bidhaa za kiwanda hicho wikiendi ilopita.


No comments: