NA PRISCA MANYAMA
MAPADRI wawili wa kanisa Katoliki, wamekufa maji wakati wakiogelea katika ufukwe wa bahari ya Hindi.
Mapadri hao ambao mmoja wao ni katibu wa ubalozi wa Vatican nchini Tanzania, aliyejulikana kwa jina la Padri Degn Maxime (35), raia wa Ivory Coast, alikuwa na Padri John Rocksler (59), raia wa Ujerumani, ambaye alikuwa Mkuu wa nyumba ya Shirika la Wabenedictin iliyoko mivinjeni, jijini Dar es Salaam.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema mapadri hao walifariki baada ya kuzama na kunywa maji mengi wakati wakiogelea katika ufukwe wa hoteli ya Kasa, Kigamboni.
Misime alisema Padri John (59), alikuwa akiishi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kurasini na Mexime (35), raia wa Ivory Coast, alikuwa Katibu wa ubalozi wa Vatican nchini Tanzania.
Kamanda Misime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10.30 jioni katika ufukwe huo na kwamba, watu hao walifika hotelini hapo saa tano asubuhi wakiwa na gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T1480 AXK.
Alisema walipofika kwenye ufukwe wa hoteli hiyo, walikwenda baharini kuogelea na hivyo kukumbwa na mkasa huo, unaodaiwa kutokea kutokana na kushindwa kuogelea katika kina kirefu cha maji na kujikuta wakinywa maji mengi.
Hata hivyo, alisema maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Katika tukio jingine, moto uliozuka ghafla katika nyumba moja yenye vyumba vitatu vya ofisi, umeteketeza chumba kimoja pamoja na mali zote zilikuwemo ndani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 1.00 usiku, maeneo ya Mwananyamala wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Kamanda Kenyela alisema moto huo uliteketeza chumba hicho na mali zote zilizokuwamo, alizoeleza kuwa zilikuwa zinamilikiwa na Dk. Ashock Salum na Tina Urera.
Chanzo cha moto huo na thamani ya vitu vilivyoungua bado haijafahamika.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, moto huo ulizimwa na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya jiji, kikisaidiwa na majirani wa eneo hilo, na kwamba hakuna madhara yoyote kwa binadamu.
Mohamed Bouazizi (26) alifariki dunia juzi jioni hospitalini nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis. Kabla ya kifo chake jamaa huyo alikuwa akiuza matunda na mboga mboga kinyume cha sheria katika mji wa sidi Bouzid baada ya kukosa ajira. Mwezi uliopita aliamua kujimwagia mafuta ya petrol na kujitia kiberiti baada ya polisi kuharibu bidhaa zake kutokana na kutokuwa na kibali maalum.
Zaidi ya watu 5000 walihudhuria Mazishi yake huku waombolezaji wakisema "KWAHERI MOHAMMED sisi tutalipiza kisasi kwa ajili yako. Sisi leo tunalia kwa ajili yako, tutawafanya wale ambao wamesababisha kifo CHAKO WALIE"
Polisi walilazimika kuzuia umati mubwa uliofika nje ya ofisi ya gavana ambako bw. Bouazizi alijilipua. “Muhammad alitoa maisha yake kwa kuonesha uchungu na hali yake na kwa ndugu zake”
Ghasia hizo zilisababisha mwandamanaji mmoja kuuawa baada ya polisi kufyatua risasi
No comments:
Post a Comment