Wednesday, February 16, 2011

TASNESCO wahaha na mgawo wa umeme


Na Lilian Timbuka

SHIRIKA la Umeme nchini, Tanesco, sasa limenunua mafuta ya kuendeshea mtambo wa umeme wa IPTL uliopo, Tegeta, Dar es Salaam, ili kuzalisha megawati 80 kwa siku, ikiwa ni moja ya hatua zake kujaribu kupambana na mgawo wa umeme ambao shirika hilo limekiri kuwa unalipunguzia heshima kwa umma.
Akizungumza na waandshi wa habari , kwenye makao makuu ya Tanesco, Ubungo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Injinia, Felchesmi Mramba,(Pichani), alisema, mafuta yameshanunuliwa na yameanza kuwasili IPTL, ili kuzalisha kiasi hicho cha megawati za umeme kwa siku.
"Hii itapunguza mgawo wa umeme kwa sasa kwa megawati zipatazo 70", alisema Injinia huyo ambaye alifuatana na Meneja Uhusiano wa Shiruika hilo, Badra Masoudi (kulia) na kuongeza "tunatarajia kwamba msimu wa mvua za masika utaanza punde, na hii itafanya uzalishaji wa umeme katika mitambo ya maji kuongezeka na hivyo kuliondoa tatizo hilo kwa sasa.
"Pia Shiruka linawasiliana na serikali kuangalia uwezekano wa kupata mit ambo ya dharura ili kukabiliana na hali inayoweza kujitokeza endapo mvua za masika zitakuwa chini ya wastani unaotarajiwa", akasema Injinia Mramba.
Akasema, uongozi wa Tanesco unawaomba radhi sanaaaa, wananchi kutokana na usumbufu mkubwa unaotokana na adha ya mgawo huo wa umeme na pia Shirika linawasihi wananchi kushirikiana na shirika hilo, na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha upungufu wa umeme.
"Tunaahidi kwamba tutafanya kila jitihada kurekebisha mapungufu balimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hapa na pale katika utekelezaji wa zoezi hili la mgawo hasa kudhibiti matukio ya dharura yanayofaya ratiba zisifuatwe kama zilivyopangwa", akamaliza..

No comments: