Sunday, March 13, 2011

BONANZA LA VYOMBO VYA HABARI LILIVYOFANA KATIKA FUKWE ZA CINE CLUB JIJINI DAR ES SALAAM MWISHONI MWA WIKI.

MCHEZAJI wa timu ya mpira wa kikapu ya Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Lilian Timbuka nikiwa katika harakati za kutumbukiza mpira katika kikapu, wakati tulipopambana na timu ya Global Publications. Katika mchezo huo Uhuru tulilala kwa bao 3-2.

GOLIKIPA wa timu ya Uhuru, Said Ambua akipangua moja ya penalt katika mchezo wa robo fainali kati ya Uhuru na Global Pulbications. Uhuru ilitolewa kwa mabao 3-2. WANENGUAJI wa bendi ya Twanga Pepeta wakiwajibika jukwaani, katika bonanza la waandishi wa habari lililofanyika juzi katika ufukwe wa Sun Club, Msasani. Bonanza hilo lilifadhiliwa na kampuni ya bia ya TBL.

WAANDISHI wa vyombo mbalimbli vya habari wakiserebuka katika bonanza hilo.

MWANDISHI wa habari wa kampuni ya Uhuru Publication Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Halima Ramadhani, akishindana kucheza muziki na waandishi wa vyombo vingine vya habari. Katika shindano hilo, Halima alishika nafasi ya pili.

WAANDISHI wa habari wa Uhuru pamoja na redio Uhuru, wakishangilia baada ya timu ya Uhuru kupatakikombe cha ushindi jumla katika mashindano hayo. aliyeshika kikombe kidogo ni Bi. Samira Kiango ambaye alipata kikombe baada ya kushinda mbio za wanawake huku akifuatiwa na Salome pia wa Uhuru FM.

Wadau kutoka Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, waki-chat, pembezoni.

Wadau wakiongozwa na Mzee wa Channel Ten Kibwana Dachi (Kushoto), wakifuatilia kwa makini kila kilichokuwa kikiendelea fukweni hapo, huku mezani kukiwa kumesheheni bidhaa za kampuni ya TBL.

Kushoto ni muandaaji wa Blog ya Chachandu Daily, Bashiri Nkorom, akiwa na wadau Athumani Hamis, Amina Molell na Faza Kidevu, wakifurahia matukio yaliyokuwa yakijiri.

Hawa nao walikuwepo ni muandaaji wa kipindi cha 'Amplifaya' cha Radio Clouds FM, Milady Ayo(Kushoto) na mtaalamu mwenzake Anselim Ngaiza a.k.a 'Sog dog' wa Uhuru Fm.

No comments: