Thursday, March 10, 2011






Mchuchuma kufua umeme Megawati 600

Na Bazil Makungu Ludewa
KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madili imeshangazwa kusikia kuwa Makaa ya mawe ya Mchuchuma peke yake yanaweza kufua umeme wa uhakika nchini kwa muda wa miaka mia moja na sitini (160) na kuondokana na adha ya nishati hiyo inayoendelea kulisumbua Taifa kwa mgawo kila kuchapo.

Dr Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mbunge msitaafu wa jimbo la kwera Mkoani Rukwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi katika Shirika la Taifa la Maendeleo nchini (NDC) aliyasemahayo jana kwenye kamati hiyo ya Bunge ilipotembelea kujionea hali halisi iliyopo Mchuchuma, Ketawaka na Liganga Ludewa.

Mzindakaya aliiambia kamati hiyo kuwa makaa yam awe ya Mchuchuma na Liganga yamecheleweshwa na watoa maamuzi kwa kuingiza siasa kwenye utendaji kwa kuwa tegemezi kwa watu wan je.Tulikuwa tunafanya makosa makubwa kutegemea wageni kwa kila kitu badala ya kufanya sisi wenyewe, aliongeza.

“mimi ningekuwa mwamuzi mwenyewe bila kuingiliwa na mtu Mchuchuma ingeanza hata kesho kwa sababu ndani ya kichwa change hakuna harufu ya epa wala Richmond.na mambo hayo ndiyo yametawala ndani ya vichwa vya viongozi waliowengi na ndiyo maana kila mtu anahofu hakuna aliye tayari kuthubutu,” alisikitika Mzindakaya

Akijibu swali la Zito Kabwe Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini aliyetaka kujua kwa kipindi chote viongozi waliotangulia akiwemo yeye mzindakaya walikuwa wapi mpaka Taifa linaingia kwenye giza. Mzindakaya alisema tulicheleweshwa na watoa maamuzi waoga.

Alisema mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Ketewaka na Chuma cha Liganga tutahakikisha mali hiyo inalindwa kwa maslahi ya umma,hatutaruhusu mwekezaji yeyote kupata kiasi kikubwa huku Serikali ikiambulia sehemu ndogo ya pato linalopatikana katika miradi mingi hapa nchini.ni lazima tupate asilimia hamsini kwa hamsini kwa sababu sisi ndiyo wenye raslimali tofauti na awali ambapo tulikuwa tukiibiwa kwa visingizio vya mtaji na teknolojia.

Mwenyekiti huyo wa bodi aliiambia kamati ya Bunge kuwa Tanzania tumekuwa tukinyonywa na wawekezaji kwa sababu hatujui kilichopo katika migodi yetu alisema zamani waingereza walitudanganya kuwa Mchuchuma ilikuwa na tani m.40 lakini tulipofanya wenyewe kwa ktumia wataalamu wa ndani tuligundua kuwa tunazo zaidi ya tani 1.2 bilioni.

Bila Mkaa wa Mawe wa Mchuchuma na Ketawaka hakuna Liganga kwa hiyo tuliweka masharti kwa wawekezaji kuwa atakayetaka kuwekeza Liganga lazima lazima awekeze na Mchuchuma kwa sababu miradi hii inategemeana, na katika mrdi huu tulishindanisha makampuni kumi na nne.

Akitoa maelekezo na ushauri kwa NDC Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Bw Zito Kabwe alisema kuwa huu ndiyo mwisho wa porojo lazima sasa wananchi waone kweli Liganga na Mchuchuma imeanza kutoa matunda na mawasiliano yafanywe kila mara kati ya kamati hiyo na NDC.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mkomang’ombe kwenye Mkutano wa hadhara alisema kuwa kamati hii imekuja kuhakisha maendeleo yanapatikana ndani ya Ludewa na Taifa,yale maneno ya michakato yamekwisha tumeshatoa maelekezo kwa wahusika.

No comments: