Monday, July 23, 2012

Dk. Sheini aongoza viongozi
katika dua maalum ya hitma

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar. Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume. Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine. Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume. Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.


Airtel yatoa msaada wa vitabu Singida

Airtel yatoa msaada wa vitabu shule ya secondary Mtipa wilaya ya
Singida Mjini - Singida Dar Es Salaam, Jumapili - Julai 22nd 2012,
Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora
nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari
Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.
Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel
mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya
Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo
bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma
kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni. Shule imepewa msaada wa vitabu
vyenye thamani ya shilling milioni mbili.
Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia,
Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.
Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za
Airtel mjini Dar Es Salaam Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania
Hawa Bayuni alisema" Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia
jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini
Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya
sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika
katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa
shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya
Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani
tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya
kesho. Aliongeza Bayuni.
Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo
fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu
nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni
kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka
graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu
vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika
kutimiza malengo tuliojiwekea.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa
msaada wa kutoa computer 4 na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano
kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini.
Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika
huduma kwa jamii.


Sh. milioni 10 zatengwa
kufuturisha Dar es Salaam

Zaidi ya sh milioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kufuturisha watu wenye kipato cha chini kwenye mwezi huu wa mfungo wa Ramadhani katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaa leo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Madina, Sheikh Ally Mubaraka alisema hayo wakati alipokuwa akipata futari kwa pamoja na waislamu wa Msikiti wa Sheikh Gorogosi, Tandika kwa Maguruwe.
Alisema fedha hizo zimepatika kutokana na ushirikiano mzuri uliyopo kati ya Ubalozi wa Emirate na taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji misaada katika jamii yenye mahitaji maalum.
Sheikh Mubaraka alisema taasisi hiyo inalenga kutoa futari kwenye makundi ya watu ikiwa ni ishara ya huruma kama dini hiyo inavyoelekeza.
“Ubalozi wa Emirate umejitolea fedha za kutosha kwa ajili kufuturisha ambapo leo (jana), tumeanzia Tandika, mpango huu ni wa kila mwaka na utafika katika maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam”alisema Sheikh Mubaraka.
Sheikh Mubaraka aliwaasa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei za bidhaa kwa ajili ya kujipatia kipato kikubwa ambapo sheria za dini zinawataka wanadamu kuoneana huruma wakati wote.
Vilevile alisema mwezi huu wa mfungo Ramadhani ni fursa njema ya kufanya ibada kitendo ambacho kitawasidia waislam kufutiwa dhambi zao.
“Yule mwenye kula mchana katika mfungo huu,hata kama atakuwa akijibidiisha na swala atambuwe kuwa hatoweza kufutiwa dhambi zake”alisema Sheikh Mubaraka.
Akizungumzia tukio la kuzama kwa meli ya Skagit, alisema taasisi hiyo imetoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu zao kwani tukio lile ni kubwa ambapo uchungu wake umemgusa kila mtu katika nchi hii.

No comments: