Monday, July 30, 2012

TUNU PINDA AZINDUA MRADI WA MAJI HOSPITALI YA MAWENZI

Mgeni rasmi mama Tunu Pinda akiwasili katika eneo la tukio.


Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephraim Mafuru.


Mama Tunu Pinda akipanda mti katika hospitali ya Mawenzi baada ya kuwasili hositlaini hapo kwa ajili ya uzindua wa mradi wa maji.


Mama Tunu Pinda akimsikiliza Richard Wells Mkurugenzi wa SBL wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika hospitali ya Mawenzi leo.


Wakuu wa Kampuni ya bia ya Serengeti mstari wa mbele kutoka kulia, Mkurugenzi mpya wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Steve Gannon na Teddy Mapunda, nyuma kutoka kulia John Collins Mtaalam wa Fedha, Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji na Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko.


Tunu Pinda akifunua paziana Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Richard Wells, kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi mjini Moshi, mradi huo ambao umefadhiliwa na kampuni ya SBL, umegharimu zaidi ya sh. milioni 50 na umelenga kutatua tatizo la maji lililodumu kwa muda mrefu, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dk. Msengi.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza katika uzinduzi huo huku Tunu akifuatilia kwa makini.


Baadhi ya wauguzi na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments: