* Wakacha mgomo
*Wataka taarifa ya mapato na matumizi ya michango
BAADHI ya walimu wa shule za msingi mjini Iringa wamekigeuzia kibao Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakipinga mgomo wake wa walimu ulioanza nchini kote leo na badala yake wametaka waelezwe kwanza mapato na matumizi ya michango yao ya kila mwezi kwa chama hicho.
“Tunasikia kuna majengo ya walimu yanajengwa nchi nzima, makatibu wa cwt wananuliwa magari, sasa kuna mpango wa kuanzisha benki, lakini hatupewi taarifa ya mapato na matumizi, na hata magari waliyopewa makatibu hayana msaada kwa walimu ambao ndio wenye mali hata kama wakiumwa,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mtwivilla,. Sidified Mapunda.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi y a Wilolesi ambayo pia walimu wake wote walisusia mgomo hu, George Kameka alisema kabla ya kumgomea mwajiri wao, wanataka kufahamu tangu kutoka kwa chama chao hicho cha wafanyakazi tangu walimu nchini kote waanze kukatwa asilimia mbili kwa ajili ya kukichangia, mapato na matumizi yake yakoje.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.
No comments:
Post a Comment