Monday, November 16, 2009

UPO MPAKA HAPA, FANI NI FANI TU!

MZEE BENEDICTOR AFYATUA SINGLE YAKE!!!!!!!
BABA Mtakatifu Benidicto 16, ameushangaza ulimwengu na waamini wote wa Kikristo baada ya kutoa albamu ya nyimbo za dini ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mamilioni ya watu duniani.
Hatua hiyo ambayo imewashitua watu wengi duniani, ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki Duniani, na aimeelezwa kwamba itaamsha ari ya utungaji na uimbaji wa nyimbo za dini ndani na nje ya Kanisa hilo.
Albamu hiyo itakayojulikana kwa jina la Alma Mater, na ambayo ni mahususi kwa ajili ya kipindi cha Krismas, imewashirikisha waimbaji mashuhuri Bob Dylan, Tori Amos na Sting.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Baba Mtakatifu, albamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumapili ya Novemba 29, ambapo mamilioni ya watu wanatarajiwa kushuhudia uzinduzi wake ambao utakaotangazwa karibu na mashirika makubwa ya habari duniani.
Hatua ya Baba Mtakatifu kuweka mambo mengine ya utumishi na kujiingiza katika uimbaji, imepokelewa kwa furaha na watu wengi ambao wamedai kwamba kutaimarisha zaidi moyo na ari ya uimbaji, na pia utakuza hadhi na heshima ya kwaya sehemu nyingi duniani.
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya mapadri wameeleza kuguswa kwao na hatua hiyo ya Baba Mtakatifu, ambayo wamesema imewapa nguvu za kufanya utume wao kwa unyenyekevu mkubwa.
Mmoja wa mapadri hao, Gregory Mkhotya wa Parokia ya Mt. Gaspar De Buffalo, Mbezi Beach, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, amesema hakuamini aliposikia habari hizo kwa mara ya kwanza. “Sijaamini hadi nisome. Lakini kama ni kweli, litakuwa jambo kubwa na zito kabisa kwetu sisi tuliopewa dhamana ya utumishi”
Padri Mkhotya ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo, amesema hatua hiyo imempa nguvu kubwa ya kuendelea kutunga nyimbo zaidi na kuacha kujitetea kwamba hana muda wa kuitumia karama aliyopewa na Mungu.
“ Fikiria kwamba yeye kama kiongozi mkuu ana majukumu mengi, lakini bado ametumia kipaji alichopewa na Mungu kikamilifu bila choyo. Je, sisi tunaosimamia waamini wachache tuna sababu gani ya kutotumia karama zetu kikamilifu kwa kisingizo cha kubanwa na majukumu?
Alisema Padri Mkhotya.
Imeelezwa kwamba mauzo ya albamu hiyo siku ya uzinduzi huenda yakavunja rekodi za albamu zote zilizowahi kuuzwa siku ya uzinduzi, nah ii inatokana na ushiriki wa mtu mzito katika ngazi ya uongozi wa Kanisa.

No comments: