Sunday, November 28, 2010



Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Bi. Salome Maro ambaye ni Mwanachuo aliyefanya vizuri na kupata daraja la kwanza akiwa na GPS 4.5 katika kozi ya Computer Science kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Waziri Mkuu Alikuwa Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Sherehe za Miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam iliyofanyika katika ukumbi wa Nkrumah leo.


Chuo Kikuu Cha Dodoma leo kimewatunuku Shahada ya Heshima ya
Udaktari (Doctor Honoris Causa) Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa kutambua michango yao mbalimbali katika Nyanja za siasa na sekta za elimu nchini ikiwemo kuasisi ujenzi wa Chuo hicho. Pichani ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, akimtunuku shahada ya Heshima ya Udaktari Rais Dr.Jakaya Kikwete wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho iliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma leo. Katikati ni Makamu mkuu wa Chuo Profesa Idriss Kikula

No comments: