Sunday, January 9, 2011




Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye akiongea leo. Shoto ni Naibu DCI Kamishna wa Polisi Peter Kivuyo.




Kamishna wa Operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi Afande Paul Chagonja


Na Mwandishi Wetu, Arusha

Jeshi la polisi mkoani hapa limesema kuwa halijafanya kosa kuvuruga maandamano na mkutano CHADEMA majuzi likidai kuwa yangeachwa yaendelee yangeleta madhara makubwa zaidi ya yaliyotokea. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye amesema mchana huu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake kwamba jeshi hilo limetenda haki kabisa kuvuruga maandamano hayo na mkutano huo kwani iwapo vingefanyika kungeweza kutokea madhara makubwa zaidi ambayo yangewapata wananchi na mali zao. Alisema kuwa mpaka sasa vurugu hizo zimesababisha vifo vya watu watatu baada ya leo kuongezeka ameongezeka mtu mmoja ambaye alijeruhiwa siku hiyo na kusababisha idadi ya watu waliokufa katika vurugu hizo kufikia watatu. Kamanda Andengenye alimtaja mtu huyo kuwa ni Ismail Omari (37) mkazi wa Unga limited ambaye yeye alijeruhiwa kwa risasi tumboni katika fujo hizo. Amesema marehemu alifariki leo asubuhi katika hospitali ya mkoa ya Mounti Meru na mwili wake umeifadhiwa katika chumba cha kuifadhia maiti cha hospitali hiyo. Naye Kamishna wa Operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi Afande Paul Changonja amesema katika mkutano huo kwamba viongozi wa CHADEMA walikuwa wameachwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashitaka kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria na sio kwa kufuata shinikizo la mtu yeyote. Afande Chagonja kasema jeshi la polisi linamshangaa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kujifanya kutoa amri viongozi wa chadema watolewe na kutopewa mashariti yeyote, akisisitiza kuwa hicho ni kitu ambacho hakutegemea kabisa mtu kama yeye angeweza kuongea. "Namshangaa sana Zitto kuzungumza maneno kama haya. Anazungumza maneno bila ya kufikiria kweli, na wakati CHADEMA ndio wamesababisha haya yote. Wasilikwepe hili na wala wasitafute njia ya kulikwepa kabisa "alisema Chagonja. Alimalizia kwa kuwapa pole wale wote waliopata mazara na kusema kuwa kwa sasa wasiwe na wasiwasi kwani hali ya mji wa arusha imerudi sehemu yake na kutakuwa na fujo tena .


CHUO KIKUU CHA ULINZI WA TAIFA KUFUNGULIWA HIVI KARIBUNI

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Jeshi la Wananchi wa Tanzania litafungua Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa kitakachotoa Mafunzo ya Udhamili wa Stratejia ya Ulinzi na Usalama kwa muda wa mwaka mmoja ifikapo tarehe 10 Januari, mwaka huu katika maeneo ya kunduchi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Abdurrahman Shimbo amesema elimu hii haikuwahi kutolewa hapa nchini na waliohitaji elimu hiyo waliipata nje ya nchi.
“Elimu hii ilikuwa haipatikani hapa nchini na wote waliobahatika kuipata iliwaladhimu kwenda katika nchi za nje ambapo gharama ni kubwa sana kwa mfano mimi nimesoma elimu hii kwa fedha za kitanzania milioni 80.’’ Amesema Shimbo.
Mnadhimu Mkuu Shimbo amefafanua kuwa chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 60 kwa mwaka lakini kwa kuanzia chuo hiki kitachukua wanafunzi 20 tu.
Chuo hicho kilichoanza kujengwa Machi mwaka jana na kumalizika Desemba mwaka huo huo ni mahsusi kwa maofisa wa ngazi za juu za polisi, uhamiaji na jeshi.
Kufanikishwa kwa ujenzi huo kumetokana na ufadhili wa Serikali ya Tanzania na china ambapo mpaka sasa Tanzania imetumia kiasi cha fedha za kitanzania bilioni mbili na china imetoa takribani dola za kimarekani bilioni tatu.


Mh. Nyalandu akiangalia dagaa waKigoma sokoni Kariamoo shimoni
Wafanyabiashara ndogondogo ‘wamachinga’ wa kigeni wametakiwa kuondoka ndani ya siku 30 ili kuacha watanganyika kufanya biashara hizo.
Naibu Waziri wa Biashara an Viwanda, Lazaro Nyalandu alisema jana wakati alipotembela soko kuu la Kariakoo jijini Dar kuwa wageni wote kutoka nchi za Asia na Afrika wanaojihusisha na biashara hizo waache ama wafuate taratibu za uwekezaji nchini.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa wamachinga kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika na Asia kufanya shughuli hizo kinyume na vibali vyao,jambo ambalo linawanyima fursa wazalendo kufanya kazi hiyo.
Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi kwenye soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam jana,Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko,Lazaro Nyalandu alisema kuwa, idadi kubwa ya wageni hao kufanya shughuli hizo kinyume na taratibu imesababisha serikali kukosa mapato.
Alisema,kuna baadhi ya wafanyabishara wameomba kibali cha uwekezaji,badala yake wameshindwa kufanya hivyo na kuanza shughuli za umachinga huku wakiwaita ndugu zao kinyume na taratibu, kutokana na hali hiyo serikali haitawaacha, itawashughulikia.
“Wale wote wanaofanya shughuli za umachinga kinyume na vibali vyao waache mara moja na kuondoka nchini kwao kabla yakuchukuliwa hatua za kisheria, kutokana na hali hiyo watendaji weote watapita kwa kila wafanyabishara kwa ajili ya kufanya ukaguzi,”Alisema Nyalandu.
Aliongeza watanzania ambao na wenyewe wamejifanya kuwa wao ni wenyeji wa wageni hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ili Tanzania isionekane dampo la wafanyabiahsra wanaokwenda kinyume na sheria.
Alisema kuanzia sasa watendaji wa idara ya biashara watazunguka kwenye masoko yote kwa ajili ya kukagua vibali vya wafanya biashara hao na kuwaorodhesha ili waweze kubainika ni wa ngapi na wamekuja kufanya kazi gani.
Kwa mujibu wa Nyalandu,baadhi ya watu wanajifanya madalali wa kuwakaribisha wageni hao na kuwaingiza kwenye shughuli hizo kinyume na taratibu, jambo ambalo linasababisha serikali kukosa mapato, kutokana na hali hiyo watu hao watashughulikiwa.
Alibainisha, soko la kariakoo ni miongoni mwa maeneo yaliyojaa wageni hao, jambo ambalo limesababisha baadhi ya wazalendo kukosa nafasi ya kufanya bishara hizo.
Alibainisha,serikali kwa sasa inafanya mazungumzo na serikali ya China ili waweze kudhibiti baadhi ya wafanyabishara wasio waadilifu ambao wamekuwa wakiingiza bidhaa feki zinazohjatarisha maisha ya wananchi.
“Kuna mazungumzo kati yetu na serikali ya China kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia, lengo ni kuiondoa Tanzania kuwa dampo la bidhaa hizo,kutokana na hali hiyo bidhaa zitakazokuwa zinaingia zitakuwa na ubora unaokubalika,”alibainisha.
Aliongeza kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kuwa makini na wafanyabishara wa bidhaa bandia kwa akuangalia ubora wa bidhaa hizo na mahali ilipotoka.

No comments: