Tuesday, July 31, 2012

Airtel money sasa bure

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (pichani), alisema "Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa na mengine mengi

tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja

vilevile tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi aliongeza” Mmbando

Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma za kibenki.

Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi

Kupata huduma ya Airtel money sasa piga *150*60# Bure



CBA YAIPIGA TAFU SMZ UNUNUZI WA MELI


Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta fedha za kununua meli mpya, Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), imesema iko tayari kuikopesha SMZ fedha za kununulia Meli hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Yohane Kaduma, amesema benki yake iko tayari kuipitia SMZ mkopo wa kununulia Meli hiyo endapo watakubaliana na kushirikishwa kwenye mchakato huo.

Bw. Kaduma alikuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zannzibar mara baada ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 5, kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibat Balozi Seif Ali Iddi ili kusaiidia ghala za matibabu kwa majeruhi na ubani kwa wafiwa wa ajali ya Meli ya Skagit.

Bw. Kaduma amesema kuwa endapo Benk yake itaombwa kutoa mkopo huo inaweza kufanya hivyo ili mradi tu kukaa meza moja na Serikali na kukubaliana aina ya mkopo pamoja na mambo mengine.

Awali akipokea msaada huo, Makam wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, amesema kuwa pamoja na kusimamishwa kwa baadhi ya meli za watu binafsi kuchukua abiria, SMZ pia imeagiza meli zake kufanyiwa uchunguzi kama zinafaa kuchukua abiria.

Balozi Seif amesema kuwa ameziagiza Mamlaka ya usafiri majini Zanzibar na Sumatra, kuzifanyia uchunguzi meli hizo za SMZ ikiwemo MV Maendeleo ambayo imerejea siku za karibuni ikitokea Mombasa nchini Kenya ambako ilikuwa katika matengenezo makubwa.

Amesema Serikali haiwezi kukaa kimya huku ikiona kuwa wananchi wake wanapatwa na majanga ya mara kwa mara kutokana na kusafiri kwa meli zisizo na uhakika.


Afisa Mtendaji mkuu wa benki ya CBA, Bw Yohane Kaduma akimkabithi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh Millioni 5 kwa makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Idd, Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Bw Kaduma amesema benki yake iko tayari kuikopesha serikali ili iweze kununua meli mpya ili kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri majini.Nae balozi Seif Idd ameshukuru msaada huo kutoka CBA na ametoa wito kwa wadau mbalimbali na serikali kuitembelea benki hiyo ili kuona ni jinsi gani taifa linaweza kufaidika hasa kwenye kuisaidi serikali kuboresha usafiri majini

Katika hatua nyingine idadi ya maiti za MV Skagit, imeongezaka hadi kufikia 128 baada ya maiti nyinine mbili kupatikana leo karibu na Kisiwa cha Chumbe nje kidogo ya mji wa Zanzibar na nyingine sita zikipatikana mkoani Tanga.

Tofauti na taarifa za awali kuwa maiti tano zilipatikana Bagamoyo mkoani Pwani, ifahamike kuwa maiti hizo zilipatikana katika fukwe za bahari wilayani Pangani na nyingine mjini Tanga.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Tanga ACP Costantine Masawe, maiti nne ikiwemo ya mwanamke mmoja zilipatikana huko Pangani na nyingine mbili ikiwemo ya mwanamke mmoja zikapatikana kwenye fukwe za bahari mjini Tanga.

Kamanda Masawe amesema kuwa maiti zote zilichukuliwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa Vinasaba (DNA) pamoja na kupigwa picha kabla ya kuzikwa.

Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa maiti moja kati ya hizo, ilitambuliwa kuwa ni ya Mohammed Saidi Salum mkazi wa Ziwani Chakechake mkoa wa Kusini Pemba ambaye alitambuliwa baada ya simu aliyopatikana nayo kufanyiwa uchunguzi.

Hadi sasa maiti ambazo hazijapatikana ni 16 kutokana na kupatikana kwa watu 146 wakiwa hai ikilinganishwa na idadi ya watu 290 waliokuwemo ndani ya meli hiyo ya Skagit siku ya tukio.

No comments: