JITOKEZENI KWA WINGI SHEREHE YA MASHUJAA
WANANCHI wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012 jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Amesema katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam baadhi ya barabara zitafungwa ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi Mohamed ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaohudhuria maadhimisho hayo na kuongeza kuwa katika kuboresha maadhimisho hayo kamati ya maadhimisho itaweka luninga katika maeneo yote muhimu ili kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka wakati wa maadhimisho hayo.
Aidha Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.
“ Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu sana katika historia ya nchi yetu kwani tunawaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa, kuilinda na kudumisha amani na utulivu wan chi yetu.”
Askari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa Julai 25 wakiendelea na mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Askari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa Julai 25 wakiendelea na mazoezi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment