Tuesday, July 24, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA VIUNGA VYA BUNGE JANA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Habari. Vijana , Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 23, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mpanda Kati , Said Arfi na Mbunge wa Viti Maalum, Agripina Buyogela, Kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma July 23,2012.(Picha naOfisiya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma jana.

YANGA CHUPU CHUPU KWA MAFUNZO, YAFUZU NUSU FAINALI


Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kufuzu kusonga mbele hatua ya nusu fainali jana baada ya kuishinda kwa mbinde timu ya Mafunzo toka Zanzibar kwa mikwaju ya penarti

YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-3, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yanga wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.

Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.

Katika mchezo huo, Juma Othman Mmanga alipoteza fahamu na kuwaweka roho juu wachezaji wenzake na mashabiki, akatolewa nje akipepewa na hakuweza kuendelea na mchezo, lakini taarifa za baada ya mchezo zilisema anaendelea vizuri.

Kipa wa Yanga Berko aliumia dakika ya 69 na akatibiwa kwa dakika tatu, kabla ya kutolewa nje dakika ya 72, nafasi yake ikichukuliwa na Ally Mustafa Barthez ambaye ukaaji wake mazuri langoni wakati wa penalti ulimfanya Said Mussa Shaaban wa Mafunzo akapiga nje na kuipa Yanga ushindi.

Saidi Bahanuzi alipiga penalti ya kwanza, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ya pili, Hamisi Kiiza ya tatu, ya nne Haruna Niyonzima na Athumani Iddi ‘Chuji’ alipiga ya mwisho na kuwainua maelfu ya mashabiki wa Yanga Uwanja wa Taifa.

Timu zilivyopangwa;

YANGA SPORTS CLUB

Yaw Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika/Idrissa Assenga, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo/Jerry Tegete.


MAFUNZO


Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir na Ally Juma Hassan.



WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AMALIZA ZIARA YAKE MAREKANI


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Sued Kagasheki akimkabidhi tuzo ya kinyago Bi. Jena Fox, mwanahabari kutoka Jarida maarufu la nchini Marekani la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni. Tuzo hii ilitolewa na Bodi ya Utalii nchini kufuatia uandishi mzuri wa makala mbalimbali za kutangaza ukanda wa utalii wa kusinikatika soko la Marekani.



Waziri Kagasheki akifanya mahojiano na mwanahabari Jena Fox kutoka jarida la Travel Agent Magazine la jijini New York hivi karibuni. Katika mahojiano hayo, alipata fursa ya kuelezea fursa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.



Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini, Dk. Sloyce Nzuki, akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Wageni cha Marekani (USTOA), Peggy Murphy, baada ya kufanya nae mazungumzo juu ya namna ya kuongeza idadi ya wageni nchini kutoka Marekani, jijini New York hivi karibuni.





No comments: