YALIYOSISIMUA
Somalia kufundisha uanzishaji chama
Makamu wa kwanza wa Rais wa Somalia, Hussein Kummie amesema serikali ya nchi yake ina kazi kubwa kuwafundisha wananchi mjini na vijijini maana ya mapinduzi ya nchi hiyo ili baadaye wawe katika hali ya kuanzisha chama cha kuendesha serikali yao wenyewe.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha UNIP cha Zambia, Ruben Kamanga alisema Zambia inaamini kuwa nchi za Afrika zitasaidiana kila wakati nchi nyingine zitapokabiliwa na matatizo na kuitaka 'AFRIKA HURU' kulitazama kwa makini tatizo la kwea kutambua kwamba uchafunzi wa uongozi wa wananchi wenye wa Angola.
Kwa upande wake, Rais wa ANC ya Zimbabwe, Askofu Abel Muzorewa, alitoa mwito kwa nchi huru za Afrika na zile zinazopenda amani duniani kukisaidia chama chake katika vita ya ukombozi na akaahidi kuwa kila msaada utakaopatikana utatumika kwa ajili ya lengo la kufikia uhuru.
Vyama vingine vilivyotoa salamu za pongezi kutoka India ,Misri, Urusi, Syria, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Yemen, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani, Malawi, Tunisia, Rwanda na Yugoslavia.
Mkutano utaendelea leo asubuhi na kazi ya kwanza itakuwa kuunda kamati za kuzingatia majadiliano ya mkutano na baadaye itafuata kazi kufanya masahihisho ya katiba na jioni kupokea na kujadili ripoti za idara za chama.
Naye Makamu wa Rais wa TANU, Rashidi Kawawa alisema kuwa ingawa hivi sasa kuna vita vikubwa vya kupambana na hali mbaya ya uchumi duniani, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hazitaweza kufanikiwa iwapo wananchi hawatashirishwa barabara katika suala hilo.
Kuhusu vita vya ukombozi, Kawawa alisema kwamba kama wana Afro Shirazi walivyoahidi, wana TANU nao watashikana bega kwa bega na wapenda amani duniani kusaidia juhudi za ukombozi katika sehemu ambazo zinakaliwa na wapinzani.
Akitoa salamu za chama cha nchi yake, mjumbe wa FRELIMO, Felisto Lukanga, alisema anaamini maazimio ya mkutano huo yataimarisha mapinduzi ya Zanzibar na akatoa wito kwa nchi zinazopenda amani kusaidiana kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Angola.
Hiyo ilikuwa Novemba 20, 1975
Friday, July 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment