Utawala wa sheria! unaheshimu haki za binadamu?
Na Lilian Timbuka
WAKATI Tanzania ilipokuwa ikitaka kuingia katika mchakato wa mfumo wa vyama vingi vya siasa, Serikali haikuweza kujitolea maamuzi, bali iliwataka Watanzania kutoa maoni yao juu ya mfumo huo.
Hata hivyo Watanzania wengi walionesha kutounga mkono na wengi wao walionekana bado kupendelea mfumo wa chama kimoja.
Hali hiyo binafsi ndio naona iliyosababisha kutopata uungwaji mkono kwa kiasi cha kuridhisha kwa vyama vya siasa hapa nchini kwa asilimia kubwa kama baadhi ya watu walivyokuwa wakitarajia.
Hata hivyo kwa uapnde mwingine, huenda hali hii ikawa inasababishwa na kutokuwapo na changamoto ya kutosha kwa vyama hivi ambavyo bado havina nguvu ya kutosha kuweza kuungwa mkono na asasi za kiraia ambazo nazo bado ni dhaifu.
Madaraka mengi na makubwa tunashuhudia yakiwa bado mikononi mwa serikali kuu ambayo iko chini ya chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wakati nchi inapiga hatua pole pole ya kuelekea maendeleo ya kidemokrasia na utawala bora, hali za watu kimaisha, bado zinaonekana duni, licha ya kuwepo kwa takwimu rasmi zinazoonesha ukuaji wa wastani wa kiuchumi, na pengo baina ya maskini na matajiri.
Kwa wastani nchi bado inakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kutokuyakinisha juu ya utawala bora na mfumo wa kidemokrasia katika nchi, kutokana na kunonekana kwa asasi fulani za utawala kuwa na nguvu katika kuimarisha mfumo wa kidemkorasia na uwajibikaji ambako kunasababisha kujitokeza kwa hisia miongoni mwa baadhi ya raia na hasa viongozi kama vile zinahatarisha usalama, amani na umoja wa kitaifa.
Juhudi za kujiletea maendeleo ya kichumi nako kunadorora pia.
Katika muktadha huo, Dk. Mohammed Bakari Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipozungumza na Mwandishi wa Makala haya, alisema kuna haja kubwa ya kutafakari kwa kina juu ya uhusiano uliopo baina ya utawala na usahihi baina ya utawala bora wa kidemokrasia na maendeleo. Alisema kinadharia, Watanzania wanazungumza zaidi kwa kifupi uhusiano kati ya utawala na maendeleo pamoja na umuhimu wa demokrasia katika kuwezesha maendeleo ya kiuchumi.
Dk. Bakari aliongeza kuwa uainishaji huo unapaswa kulenga katika aina gani ya maendeleo inahitajika katika ngazi ya kitaifa na ngazi za chini, na mwisho asasi za utawala yaani Serikali za Mitaa, katika ngazi ya chini ambazo zinapaswa zijue zifanye nini ili kuwezesha uanzishwaji wa demokrasia wenye lengo la kuleta maendeleo.
Hata hivyo historia inaonesha kuwa, toka mwanzoni mwa miaka ya 80, dhana ya utawala au utawala bora, zimekuwa zikitumika sana miongoni mwa wanataaluma na watunga sera katika nchi zote duniani, zilizoendelea na zinazoendelea sanjari na zile za kidemokrasia na zisizokuwa za kidemokrasia.
Lakini pamoja na kuwepo kwa mijadala ya kitaaluma, tafiti na machapisho mbalimbali juu ya utawala na utawala bora, hayajapata muafaka juu ya dhana inayokubaliwa na wote.
Hali hii ndio inayosababisha kuwepo kwa uhuru mkubwa wa watumiaji, lakini vile vile inaleta ugumu katika kuanisha vigezo vyake katika utendaji hai. Lakini Dk. Bakari anabainisha kuwa cha msingi ni kutanabaisha kwamba dhana hii hutegemea pia na mazingira halisi inayotumika pamoja na lengo kuu katika kutoa tafsiri na kubainisha vigezo vyake.
Alisema kulingana na matakwa halisi ya jamii husika, kwa mfano mkazo unaweza kuwekwa zaidi katika utawala wa kisiasa au utawala wa kiuchumi au mambo yote mawili yakaenda pamoja, lakini katika vipaumbele vinavyokaribiana au kulingana.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya siasa wanasema utawala bora ni dhana pana ambayo inaweza kupambanuliwa vizuri na kueleweka kwa kuangalia sifa ama vigezo vyake.
Ingawa wanataaluma na watunga sera pamoja na raia wanaweza kutofautiana juu ya dhana na sifa za utawala bora. Wanadai kuna sifa ambazo zinaweza kukubaliwa na wengi, na miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na ile ya ushiriki katika maamuzi, uatawala wa sheria, uwajibikaji na uwazi katika michakato na asasi za utawala, usawa, uhalali wa utawala na umadhubuti na ufanisi wa sekta ya umma.
Dk. Bakari anasema katika mfumo wa utawala bora, raia wote wake kwa waume lazima wawe na haki na wasaa wa kushiriki katika maamuzi muhimu yahusuyo maisha yao.
Anasema bila ushiriki mpana wa raia wote, hapa panakuwa hakuna dhana ya utawala bora wa kidemokrasia.
Aliongeza kuwa, ushiriki unaweza kuwa wa moja kwa moja au kwa kupitia katika vyombo vya uwakilishi.
Kutokana na hali hiyo, ni wazi kuwa hivi sasa kuna kubwa ya kutambua matakwa na utsahi wa makundi yasiyokuwa na nguvu katika jamii, kuwa yatawakilishwa na kutetewa ipasavyo katika maamuzi. Na lamsingi katika hili, ni kule kutambua kwamba, ushiriki ni olazima uwe na taarifa zinazostahili na ziratibiwe vizuri. Kwani ushiriki wa mtu mmoja mmoja au wa makundi madogo madogo unaweza usiwe na athari kubwa katika kufikia maamuzi muhimu ya utawala.
Hii maana yake ni kwamba uhuru wa kumuika na kujieleza kwa upande mmoja na uwepo wa asasi makini za kiraia ni mambo muhimu katika kuhakikisha ushiriki makini.
Kwa maana nyingine, utawala bora unahitaji kuwepo na kuheshimiwa kwa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki za wachache. Hili linawezekana pale ambapo kuna misingi imara ya kisheria ambayo inasimamiwa na kutekelezwa bila ya upendeleo.
Ni wazi kuwa hakuna asiyefahamu kuwa usimamizi na utekelezaji wa sheria unahitaji uwepo wa mfumo wa mahakama zilizo huru na jeshi la polisi linalofanya kazi zake kiuewa bila ya kuathiriwa na rushwa. Tunaposema utawala wa sheria, basi ni lazima uheshimu haki za binadamu!

No comments:
Post a Comment