Askofu anusurika kuuawa
WATU wasiojulikana wamekula njama za kutaka kumuua askofu mmoja wakati wa maadhimisho ya sherehe za Krismasi mwaka huu, ambapo inasemekana baada ya jaribio hilo kushindwa, waliwaua watu saba kwa wakati mmoja.
Habari za kuaminika zimesema kuwa mtu mmoja aliyekuwa na silaha na anayeaminika kuwa Mwislamu wa msimamo mkali, aliwatwanga risasi watu hao saba waliokuwa wakijiandaa kusherehekea sikukuu ya Krismasi mwaka huu.
Aliyetakiwa kuuawa ni Askofu Amba Kirollos, wa Kanisa la Othodox nchini Misri, wakati wa maadhimisho ya Krismas, ambayo hufanyika kila Januari 6, ya kila mwaka na sio desemba 25, kama ilivyo katika baadhi ya nchi.
Hatua ya mauaji hayo, inakuja wakati kumekuwa na wimbi la kuwashambuliza waamini wa Kikrsto na hasa wa kiothodox yanayoaminika kufanywa na baadhi ya Waislamu wenye msimamo mkali.
Waamini wa dini nyingine nchini Misri wameilalamikia serikali ya nchi hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua za kulinda maisha na mali za watu wa imani nyingine. Waombolezaji waliokuwa katika msiba wa watu hao saba waliouawa, waliwarushia mawe polisi kuonesha hasira zao.
Hata hivyo, polisi wa nchi hiyo wanawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kula njama kupanga mashambulizi dhidi ya Wakristo.
Monday, January 18, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment