Maelfu ya Mapadri kukutana Dodoma
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya nyimbo, mashairi, Uandishi wa Insha na kongamano kubwa la mapadri ni miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu, wakati wa maadhimisho ya Mwaka wa Mapadri.
Katibu Mtendaji wa Idara ya Kichungaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Edgar Mbegu, amesema kuwa maelfu ya Mapadri kutoka kila pembe ya Tanzania, wanatarajiwa kukutana Mwezi Agosti mwaka huu mkoani Dodoma, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Mwaka wa Mapadri uliotangazwa na Baba Mtakatifu, Benedikto XVI.
Padri Mbegu amesema katika kuadhimisha mwaka huu, watu mbalimbali wamealikwa kushiriki katika maadhimisho hayo kwa kushiriki misa na ibada maalum zenye nia ya kuwaombea Mapadri ili wadumu katika wito wao katika hali ya njema.
Amesema Kanisa linahitaji nguvu na neema ya Mungu kwa wakati huu ambao dunia imekosa ladha ya utakatifu na changamoto mbalimbali zinazolikabili Kanisa. Ameongeza kwamba ustawi wa Kanisa unahitaji nguvu za pamoja baina ya mapadri na waamini kwa sababu, hakuna Padri bila familia inayoishi kulingana na neno la Mungu.
Amesema mbali na sala na misa, kutakuwa na mashindano ya kutunga nyimbo, mashairi na insha mbalimbali zenye ujumbe wa Mwaka wa Mapadri ambapo watakaofanya vyema watazawadiwa.
Amesema kila jimbo litaweka utaratibu wake wa kuadhimisha Mwaka wa Mapadri kwa kufanya mambo mbalimbali kadri wapendavyo, ambapo kitaifa sherehe hizo zitaadhimishwa mjini Dodoma wakati wa Kongamanao la Mapadri.
“Huu ni mwaka muhimu kwa Kanisa. Sote tunatambua kwamba, bila Mapadri hakuna Kanisa. Mapadri wana wajibu mkubwa na mzito wa kuwapeleka watu kwa Mungu na kazi hii siyo nyepesi, ni nzito na inayohitaji sala na maombi kutoka kwa waamini na wote wenye kumpenda Mungu´alisema mkurugenzi huyo.
Alisema, baadhi ya mapadri wanafanya kazi katika mazingira magumu na ya hatari, ambayo bila kusaidiwa na waamini walei, kazi yao itakuwa ngumu.
“Kuna sehemu ambayo, mapadri hawana nyumba zinazostahili kuishi kulingana na majukumu yao. Wengine hawana usafiri wa uhakika na hata kula yao ni shida” anasema.
Anakiri kwamba katika baadhi ya sehemu waamini wanamngoja padri ili awasaidie, wakati yeye mwenyewe akihitaji kusaidiwa. “Kuna sehemu gharama ya nauli kupeleka Misa ni kubwa kuliko sadaka inayopatikana. Sasa ni jukumu la waamini wenye uwezo, sio kuwaombea tu, bali pia kuwasaidia kwa hali na mali ili mapadri watimize wajibu wao kikamilifu”
Amesema lengo jingine kubwa la mwaka wa mapadri ni kuamsha miito miongoni mwa vijana ambao kwa sababu moja ama nyingine wameshindwa kutambua wito wao na hivyo, kutumika sehemu nyingine.

No comments:
Post a Comment