Tuesday, November 16, 2010


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Semamba Makinda(Mb.)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Semamba Makinda(Mb.)
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inatoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Anne Semamba Makinda(Mb.), kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi uliofanyika Mkoani Dodoma tarehe 12 Novemba, 2010 hivyo kuweza kuwa Spika wa kwanza mwanamke nchini.Ushindi wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) ni kielelezo cha jitihada endelevu za Sekta ya Maendeleo ya Jamii katika kuhamasisha jamii kutoa nafasi na kutambua uwezo walionao wanawake katika kushiriki nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi.Wakati jamii ikiendelea kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kumthamini mwanamke, bado kuna desturi na mila zenye madhara ambazo zimekuwa zikitweza utu na uwezo wa mwanamke katika kushiriki nafasi za uongozi na maamuzi. Ushindi wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) umekuwa kielelezo thabiti kwamba Tanzania inaendelea kuwathamini wanawake na kuwapa dhamana; maana wanaweza.Wizara ya Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto inatambua mchango wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) kwamba anastahili kuwa Spika wa Bunge maana sehemu zote alizopitia ameonesha uadilifu na ufanisi na hivyo kuweza kuaminiwa kuwa Spika wa kwanza mwanamke nafasi ambayo ni kati ya mihimili mitatu ya uongozi wa taifa.Wizara inatambua kuwa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) alikuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto kwa kipindi cha mwaka 1990- 1995 kazi ambayo aliisimamia kwa umahiri mkubwa hadi kufikia kuwepo kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto iliyopo hivi sasa.Wizara inaamini kuwa elimu ikiendelea kutolewa, jamii itaweza kujenga imani kwa wanawake na hivyo kuweza kufikia Mkakati wa kitaifa wa kuongeza Uwakilishi wa Wanawake katika Nafasi za Uongozi na Maamuzi; na wanawake kuendelea kushiriki katika kusimamia na kumiliki fursa za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika ngazi mbalimbali.Aidha, ushindi wa Mhe. Anne Semamba Makinda(Mb.) unaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye katika uongozi wake amejenga imani kuwa wanawake wanauwezo na aliowapa uongozi kamwe hawakumwangusha.Imetolewa naHussein A.KattangaKAIMU KATIBU MKUU

No comments: