Thursday, December 2, 2010



Habari Kutoka Mbeya nilizozipata asubuhi ya leo, ni kuwa, soko kuu la Uhindini katika jiji hilo limeangamia kwa moto kama inavyoonekana katika picha hii ya ripota wa Globu ya Jamii aliyeko katika eneo la tukio.





Hivi ndivyo soko la Mbeya uhindini linavyo onekana kwa sasa. Kwa hakika walio kuwa na maduka makubwa wote wameathirika kwa kiasi kikubwa sana na janga hilo la moto. Maduka makubwa sokoni hapo likiwemo la Mushi na Nanetelecomunnication yanayo angalia upande wa Benki ya NMB Mbalizi Road hayakuambulia kitu chochote kutokana na Moto kuunguza kila kitu na kuzingira eneo lote hilo...Taarifa zaidi zitazidi kuwajia.
Picha na Ripota wa Globu ya Jamii, Mbeya.

No comments: